Mwana Kupona
155
25.
Na ufapo wewe mbee
radhi yake izengee
ndipo upatapo ndia
wende uyitukuzie
Na siku ufufu wao
na nathari nda mumeo
ndilo takalo tendewa
tauliza atakao
Kipenda wende peponi
utapeekwa dalihini
huma buddi utatiwa
kinena wende motoni
Keti naye kwa adabu
usimtie ghadhabu
itahidi kunyamaa
akinena simjibu
Enda naye kwa imani
atakalo simkhini
mkindani huumia
we naye sikindaneni
30.
Kitoka agana naye
kingia mkongowee
mahala paka pumua
kisa umtandikie
Kilala sikukuse
mwegema umpapase
mtu wakumpepea
na upepo nasikose
Kivikia simwondoe
wala sinene kwa yowe
chamka kakuzengea
keti papo siinue
Chamka si muhuli
mwandikie maakuli
kumsinga na kumowa
nakumtunda muili
Mnyoe umpalize
sharafa umtengeze
bukurata wa ashiya
mkukize mfukize
35.
Mtunde kama kijana
asioyua kunena
kitokacho na kungia
kitu changalie sana
Mpumbaze apumbae
amrie sikatae
Muungu atakutetea
maovu kiyeta yeye
155
25.
Na ufapo wewe mbee
radhi yake izengee
ndipo upatapo ndia
wende uyitukuzie
Na siku ufufu wao
na nathari nda mumeo
ndilo takalo tendewa
tauliza atakao
Kipenda wende peponi
utapeekwa dalihini
huma buddi utatiwa
kinena wende motoni
Keti naye kwa adabu
usimtie ghadhabu
itahidi kunyamaa
akinena simjibu
Enda naye kwa imani
atakalo simkhini
mkindani huumia
we naye sikindaneni
30.
Kitoka agana naye
kingia mkongowee
mahala paka pumua
kisa umtandikie
Kilala sikukuse
mwegema umpapase
mtu wakumpepea
na upepo nasikose
Kivikia simwondoe
wala sinene kwa yowe
chamka kakuzengea
keti papo siinue
Chamka si muhuli
mwandikie maakuli
kumsinga na kumowa
nakumtunda muili
Mnyoe umpalize
sharafa umtengeze
bukurata wa ashiya
mkukize mfukize
35.
Mtunde kama kijana
asioyua kunena
kitokacho na kungia
kitu changalie sana
Mpumbaze apumbae
amrie sikatae
Muungu atakutetea
maovu kiyeta yeye